Katika miaka ya hivi karibuni shirika la mambo ya Anga na Teknolojia nchini Marekani (NASA) limekua likigundua Sayari mbalimbali kama sehemu ya utafiti wao katika kutafuta sayari yenye maisha kama ya kwetu.
Wanaastronomia walisema kwamba tumeweza kugundu sayari ambayo tunaona hii ina weza kua kama dunia yetu kutokana na ukaribu wake na sayari yetu.
“Sayari hii ipo karibu na sisi ni rahisi kuifikia kwani ina umbali wa maili trilioni 25, umbali wa miaka 4 mpaka kufika”. walisema katika gazeti la New York times.
Wanaanga hao walisema katika machapisho ya jarida la “NATURE”  kwamba Sayari hiyo walioipa jina la utani “Proxima B”, imeonyesha kua na tabia kama za dunia yetu ikiwemo mfumo wa hali ya hewa, vipindi vya majira ya mwaka na hata mazingira yake yana ruhusu uwepo wa viumbe hai.
“kwa muda mwingi tulio kua tukitafuta sayari yenye kufanana kama dunia, sasa imepatikana na tuna amini kua na uweza ikawa na watu kama sisi ndani yake”. Alisema mwanasayansi katika jarida la nature.
Aidha uthibitisho wa kuepo kwa sayari hiyo kumechukua takribani miaka nane ya utafiti, huku wanaanga wakisema kwamba haikua rahisi kupata picha zake na pia ni ngumu hata kuonekana kwa macho ya binadamu kutokana na uweza wake wa kung’aa sana kuliko nyota zingine. na wamegundua kwamba proxima b, inaukubwa mara 1.3 zaidi ya dunia na ina zunguka jua lake mara moja kila baada ya siku kumi na moja.
“Hii ni kusema kwamba kuna uwezekano kabisa katika miaka ijayo tuka tuma vifaa kwenda kufanya uchunguzi na kujifunza kuhusu sayari hiyo ili kuweza kupata msaada wa kimaisha kutoka kwa majirani hao”. Alisema mmoja wa wanaanga NASA.
Na Lawdax Majani
proxima-centauri-b-landscape
proxima-centauri-b-landscape
proxima-800x533
proxima-800×533
image
earth_proxb_compared
Muonekano wa earth_proxb_