Jaji Mutungi alikuwa ahojiwe na kamati hiyo mjini Dodoma kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
Mwenyekiti wa kikao hicho, Japheth Hasunga alisema: “Tulikuwa tuwe na Msajili wa Vyama vya Siasa lakini hakuja, ameomba udhuru kwa kuwa anashughulika na usuluhishi wa vyama vya siasa.” Alisema kutokana na udhuru huo, kamati ilifanya mahojiano na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani.
Kwa zaidi ya wiki moja sasa, kumekuwa na vikao vya usuluhishi kuhusu maandamano na mkutano hiyo ya Chadema.
0 comments :
Post a Comment