Kikosi cha Jose Mourinho kinaonekana kuwa moto kwa kushinda mechi ya pili sasa tangu ligi kuu nchini Uingereza (EPL) kwa kuwachapa Southampton bao 2 kwa nunge.
Katika mchezo huo ambao Southampton alitawala kwa kiasi kikubwa mchezo huo United waliweza kupachika mabao yao kupitia Zlatan Ibrahimovic, bao la kwanza akifunga kipiti Krosi nzuri iliyopigwa na Wayne Rooney kutokea upande wa kulia huku akiongeza idadi ya mabao kwa kufunga Penalti iliyokuwa imesababishwa na mchezaji wa Southampton kumdondosha Luke Shaw ndani ya 18.
Paul Pogba ambaye ndie mchezaji anayeongoza kwa kiwango cha juu zaidi mpaka sasa katika mauzo ya wachezaji, alionesha kiwango kizuri katika mchezo huo huku akiwa mmoja kati ya vivutio vikubwa kila alipokuwa akigusa mpira.
Akizungumzia mchezo huo Kocha Mourinho mara baada ya mechi kumalizika, alisema kuwa anafurahishwa na mchezo ambao kikosi chake unakionesha na anafurahishwa na mabadiliko makubwa kwani aliikuta timu bado haijakaa sawa japokuwa kuna makosa kadhaa ambayo yanahitaji marekebisho
“Kiwango ni kizuri mpaka sasa, nafurahishwa na mabadiliko mabkubwa yanayoonekana ila bado kuna mapungufu kidogo na ni makosa tu ya kuambiana kama ukiangalia upande aliokuwa Fellain ni sehemu ya kuongea nae tu lakini pia walinzi kiujumla hawajatulia na kama southampton wangezitumia nafasi wangetuchapa nyingi sana,” alisema Mourinho
Aliongeza kuwa kwa upande wa Ibrahimovic anampongeza na anadhihirisha kwamba hakufanya makosa kumchagua, lakini pia Pogba kiwango alichocheza kuwa sio kibaya na anaamini katika michezo itakayofuata atadhihirisha thamani aliyonunuliwa.
Kwa upande wao Pogba na Ibra waliokuwa wakihojiwa kwa pamoja wamesema mashabiki watarajie kitu kizuri huku Pogba akimpongeza Ibra kwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo na akimtania kwa kufunga mabao yote mawili kwa usiku huo.
Na Derick Highiness
0 comments :
Post a Comment