Waondoeni Machinga Kwenye Barabara za DART; Waziri


Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanawaondoa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga wanaofanya shughuli za kibiashara kwenye maeneo ya barabara ya mabasi yaendayo haraka.

Sehemu ya Barabara za mabasi yaendayo haraka
Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea ripoti ya tathmini ya awali ya utekelezaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka kutoka kwa kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa, baada ya wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo kutaja uwepo wa wafanyabiashara hao kama changamoto kubwa kwa mradi huo.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mwanne Nchemba amesema maboresho yaliyopendekezwa na kamati hiyo yafanyiwe kazi kwa muda muafaka na kuleta manufaa kwa watumiaji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DART Bwana Ronald Rwakatare amesema kwa sasa wanajikita katika awamu ya pili ya usafiri huo kuelekea Mbagala ambapo utekelezaji wake utaanza mapema mwakani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment