Watanzania waliosoma China kupata uongozi mpya


C
NA  LEAH MUSHi
Chama cha watanzania waliosoma China- CHINA ALLUMNI ASSOCIATION OF TANZANIA (CAAT) hii  tarehe 27 Agosti, 2016 kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wake wapya.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rombo Green views Hotel sinza Dar es salaam kuanzia saa saba kamili mchana na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza viongozi wapya na kuwaaga viongozi waliomaliza muda wao.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa uchaguzi wa chama hicho GUSTAV SANGA uchaguzi huo utawaweka madarakani viongozi hao miaka mitatu kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Chairperson, Secretary, Treasurer, Director of Statistics, media and information, Director of Art, culture and heritage pamoja na Director of Education, Science and Technology
SANGA pia amewakaribisha watanzania wote waliomaliza China kujiunga katika chama hicho ili kuweza kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea ikiwemo kuishauri serikali masuala yahusuyo TANZANIA- CHINA.
Chama hicho cha watanzania waliosoma China kina miaka sita tangu kuanzishwa kwake na kina wanachama tangu waliosoma china miaka ya1980 kwa ngazi ya Shahada , Astashahada na Shahada ya uzamivu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment