Yanga na Azam kufungua pazia ya ligi ya TZ


Yanga dhidi ya Azam
Image copyrightALAMY
Image captionYanga dhidi ya Azam
Klabu ya soka ya Azam Fc leo imeapa kulipa kisasi katika mchezo wa kufungua pazia la msimu mpya wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa dhidi ya mabingwa watetezi Timu ya Yanga kwenye mchezo huo.
Katika mechi hiyo Azam wataingia uwanjani kwa kazi moja pekee ya kulipa kisasi baada ya mara mbili zote walizokutana katika Ngao ya Jamii kufungwa.
Afisa Habari wa klabu hiyo Jafari Idd Maganga amesema Wataingia uwanjani wakiwa na benchi jipya la ufundi linaloongozwa na Mhispania, Zeben Hernandez aliyetua nchini hivi karibuni akirithi mikoba ya Muingereza, Stewart Hall aliyesitishiwa mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Kwa upande wao Yanga kocha Hans van Pluijm amesema kikubwa yeye anataka kuendeleza rekodi yake ya kuchukua mataji kwa kuanza hili la Ngao ya Jamii.
Amesema taji hilo la Ngao la Jamii anataka kulichukua ili atengeneze mwanzo mzuri katika kulitetea taji lao la ubingwa wa ligi kuu na Kombe la FA, hiyo ni kutokana na mabadiliko makubwa ya wachezaji waliyoyaonyesha hivi karibuni baada ya kupata uzoefu mkubwa.
Hata hivyo Yanga uenda ikawakosa nyota wake watano katika mchezo huo ambao wanasumbuliwa na majeraha ambao ni Kelvin Yondan Obrey Chirwa Juma Abdul , Ally Mustapha , na Vincent Andrew .
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment