Benki inayokuja juu katika soko la fedha nchini Tanzania ya DTB (Diamond Trust Bank), asubuhi ya kesho Jumatatu saa 4.30 inatarajiwa kusaini mkataba wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuongeza udhamini katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hafla ya kusaini mkataba huo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena, iliyoko kwenye makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Ohio jijini Dar es Salaam.
Aidha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linawakaribisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kwenye hafla hiyo itakayofanyika hotelini hapo.