Ikiwa
ni michezo mitatu pekee ambayo Simba imecheza katika Uwanja wa Uhuru
ambao umeanyiawa marekebisho, Simba imeomba kurudi kutumia Uwanja wa
Taifa kama ilivyokuwa awali.
Tayari
Simba kupitia Katibu Mkuu wake, Patrick Kahemele imetuma barua kwa Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na kuomba kurudi kutumia Uwanja wa Taifa
huku sababu ya kutaka kurudi kutumia Uwanja wa Taifa kuwa ni hofu ya
usalama wa afya ya wachezaji wake kutokana na plastiki zinazoshika nyasi
katika uwanja wa Uhuru.
Sababu
nyingine ambayo imeelezwa na Simba ni uwanja kuwa mdogo, ikitolea mfano
mchezo wa Azam ambao ulipigwa Jumamosi kwa baadhi ya mashabiki wake
kushindwa kuingia kutokana na udogo wa uwanja.
Aidha
Simba imetoa ushauri kwa TPLB kuwa uwanja wa Uhuru uwekewe plastiki
mpya ili kuondoa hofu ya wachezaji wake kupata majeruhi na kama
wataruhusiwa kuchezea uwanja wa Taifa basi waanze kuujaribu mfumo wa
kieletroniki kabla ya mchezo wa Oktoba mosi ambao watapambana na Yanga.


0 comments :
Post a Comment