Kufuatia
kocha wa Manchester City, Pep Guardiola kusema kuwa hatamchezesha
mchezaji wa klabu hiyo, Yaya Toure mpaka wakala wake, Dimitri Seluk
atakapomwomba msamaha kwa kumsema vibaya, wakala huyo amemjibu.
Seluk
amesema kuwa haoni sababu ya kumuomba msamaha Guardiola kwani
anachokifanya sio sahihi na kama anataka amuombe msamaha basi aanze
Guardiola kumwomba msamaha aliye kuwa kocha Man City, Manuel Pellegrini.
“Nimwombe
msamaha kwa lipi?, Guardiola ameshinda michezo michache na anajiona
kuwa ni mfalme, ninaishi Ulaya kwahiyo naweza kusema lolote
ninalolipenda, Guardiola hawezi nizuia,
“OK,
nitamwomba msamaha Guardiola kama akimwomba msamaha Pellegrini kwa
alichofamfanyia. Kama ni mwanaume wa kweli, hilo lisingetokea.
Pellegrini alisaini mkataba mpya mwaka uliopita lakini ametolewa kwa
ajili ya Guardiola,” alisema Seluk.


0 comments :
Post a Comment