Pongezi
kwa timu ya wanawake ya Tanzania Bara ya Kilimanjaro Queens zimeendelea
kumiminika kwa kupokea salamu kutoka kwa watu, taasisi na mashirika
mbalimbali baada ya kushinda Kombe la CECAFA Woman Challenge kwa
kuifunga Kenya, goli 2-1.
Moja
ya taasisi kubwa duniani ambayo imetuma salamu kwa Kilimanjaro Queens
ni Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), kwa kutuma ujumbe wa pongezi kwa
Kilimanjaro Queens kupitia kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Salamu
za FIFA zimetumwa kupitia ukurasa wa Twitter wa FIFA Women’s World Cup
kwa kuandika “HISTORY! Congratulations Tanzania @Tanfootball, winning
the inaugural CECAFA Women’s Championship, by beating Kenya 2-1.
#KilimanjaroQueens”
Pamoja
na pongezi hizo, pia Kilimanjaro Queens imepokea salamu kutoka kwa watu
wengine akiwepo Waziri wa Michezo, Nape Nnauye, Mbwana Samatta, Thomas
Ulimwengu na kocha wa timu ya taifa ya wanaume ya Uganda, Milutin
Sredojevic Micho.


0 comments :
Post a Comment