Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa.
Nchini
Burundi duru za usalam zinaarifu kwamba mwanasiasa wa upinzani nchini
humo Gervais Niyongabo alikamatwa Jumatano kwa kosa la "kuhatarisha
usalama wa taifa". Bw Niyongabo alikamatwa mkoani Makamba, kusini mwa
Burundi.
Kwa
mujibu wa msemaji wa polisi ya Burundi, Pierre Nkurikiye, mwanasiasa
huyo kwa sasa anazuiliwa mjini Bujumbura na Idara ya Ujasusi (SNR),
ambayo ni iko moja kwa moja chini ya mamlaka ya Rais Pierre Nkurunziza.
Idara ya
Ujasusi ya Burundi inatuhumiwa na mashirika kadhaa ya kutetea haki za
binadamu kutujihusisha na mateso dhidi ya wapinzani.
Wafuasi wengi kutoka upinzani nchini Burundi wameitoroka nchi hiyo kufuatia machafuko yaliyoikuba tangu mwezi Aprili 2015.
Machafuko
hayo yalizuka kufuatia uamuzi wa Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula
mwingine katika uchaguzi wa irais uliyofanyika mwezi Julai 2015, baada
kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa muhula wa tatu, muhula ambao
upinzani unautaja kuwa ni kinyume na katibaya nchi.
Chanzo:RFI


0 comments :
Post a Comment