Mbunge
wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa
(UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa
aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea
Dotto Mwaibale
MBUNGE wa
Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000
alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya Maendeleo Endelevu aliyopewa na
Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.
Tuzo hiyo
aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili wa
tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al
Khalifa.
Akizungumza
jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja wa mataifa
umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja kupisha yale
malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo aliokuwa
wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi kikubwa.
“Tuzo
hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa, na hii
ni mara ya pili, mara ya kwanza nilipewa mwaka 2009 nchini Swideni,”
alisema na kuongeza.
“Tuzo
zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya nayo
kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa
Muleba,” alisema.
Aidha Profesa Tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo
“Sikuichukua
kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na uwezekano wa
kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani, hatuna sheria ya
kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha mezani wao
wafanye wanayotaka,” alisema na kuongeza.
“Unapoona
mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafuliwa kwenye kitu ambacho
sihusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja maadili
au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo nikawaachia,”
alisema.
Aliongeza
kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria ya
michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii visimamiwe
na si kupotoshwa kisiasa.
“Kwa
maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna
Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu
yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo
muhusu.
“Lakini
kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa uongo na
kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua hii ni
propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo,” alisema.
Aliongeza
licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado wanamfuatilia
katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa ndani na nje ya
nchi.
“Kama
ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu ni
utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi,” alisema kwa
msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.
Diwani wa
Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa wa Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Felix Bwahama ambaye
aliongozana na Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo
ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya
baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana
kimataifa.


0 comments :
Post a Comment