Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya jeshi
ya Mwenge Jazzz wana Paselepa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika
kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani jana Septemba 30,
2016
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali
Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa
wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka
52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini,
Bagamoyo mkoa wa Pwani jana Septemba 30, 2016
Ndege
vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa
Pwani jana Septemba 30, 2016
Ndege
vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa
Pwani jana Septemba 30, 2016
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali
Mohamed Shein na meza kuu wakipiga makofi wakati wa Zoezi la medani
katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani jana Septemba
30, 2016.PICHA NA IKULU.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe
Magufuli, jana tarehe 30 Septemba, 2016 amefunga maadhimisho ya miaka 52
ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani
liitwalo ”Amphibious Landing” lililofanyika katika Kijiji cha Baatini
Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Zoezi
hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano
za JWTZ ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na Jeshi
la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na
limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita yaliyohusisha kutua nchi
kavu kutoka majini na kukomboa eneo lililotekwa.
Akizungumza
baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt.John
Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis
Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki
katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa
hali ya juu.
”Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii
mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika” amesema Dkt. Magufuli.
mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika” amesema Dkt. Magufuli.
Rais na
Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ
kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na kuongeza zaidi juhudi
zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na kuwa na jeshi la
kisasa linalotumia vifaa na teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha
maslai ya askari yanaboreshwa.
Aidha, Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na kujielekeza
katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.
katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.
Maadhimisho
hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja na kuipongeza JWTZ
amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo Watanzania wanashuhudia
jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili ya kulinda nchi.
Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu
Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha
Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa
anajivunia kuwa kiongozi wa Jeshi hilo.
Maadhimisho
hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine wakiwemo Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya
Mzee.
Rais na
Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa ajira za JWTZ askari mgambo
wote walioshiriki zoezi la Amphibious Landing,
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


0 comments :
Post a Comment