Ikiwa
Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limesitisha
kuwasili makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni Jijini Dar es
Salaam kwa madai ya kutokuwepo kwa usalama na kwamba kuna vyombo vya
ulinzi vilivyowekwa kumlinda Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahim
Lipumba.
Wanaojiita
wafuasi wa Lipumba wamesema hawatamruhusu Katibu Mkuu wa chama hicho
Maalim Seif Shariff Hamadi na baraza lake kuingia katika ofisi za chama
hicho hadi atakapo kubali kumtambua Lipumba kama mwenyekiti wake.
Taarifa
ya kuaghirishwa kuwasili baraza hilo ilitolewa jana usiku na Kiongozi
wa wabunge wa CUF bara, Riziki Ngwale ambapo aliwataka wanachama na
wabunge wasiende katika ofisi hizo kutokana kwamba walifanya utafiti na
kubaini kuwa kuna wanajeshi wanao mlinda Lipumba.
Hadi muda huu, wafuasi wa Lipumba wamezingira geti kuu la kuingilia wakisubiri viongozi wa baraza hilo kama watawasili.
Mmoja
kati ya wafuasi hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, ameuambia mtandao
huu kuwa, hawataruhusu baraza hilo kuingia hadi watakapo mkubali
Lipumba.
Na
pia amesema viongozi wote waliosimamishwa uanachama watarejea katika
nafasi zao za awali akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF,
Abdul Kambaya na Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya.
Aidha,
Lipumba anatarajiwa kuongea na waandishi wa habari wakati wowote
kuanzia sasa, na kwamba yupo katika ofisi yake hadi muda huu.
Nkupamah media bado ipo katika ofisi za CUF kukuripotia kitakachojili zaidi.


0 comments :
Post a Comment