Ikiwa imepita mwezi mmoja na nusu tangu aliyekuwa kiungo wa Juventus, Paul Pogba kujiunga na timu yake ya zamani, Manchester United kwa kitita cha Euro 105, wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola amefunguka kuhusu siri ambayo watu wengi walikuwa hawaijui.
Raiola amesema kuwa kabla ya kocha Mourinho kumsajili akiwa Pogba akiwa Manchester Unite, alianza kumhitaji Pogba tangu alipokuwa akiifundisha Chelsea lakini alishindwa kujiunga kutokana na makubalianoo yaliyokuwepo ya Pogba kuisaidia kwanza Juventus kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).
“Paul alikuwa aondoke [Juventus] mwaka jana sababu ya Jose Mourinho wakati akiwa Chelsea, kweli walikuwa wakimhitaji,” alisema Raiola na kuongeza.
“Lakini mimi na Juventus tulikuwa na makubaliano, washinde ubingwa wa ligi na kombe la mabingwa Ulaya, na baada ya hapo angeondoka”