Waziri wa Mambo ya
Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua mpango
huo kwa ajili ya mikoa ya Iringa na Njombe katika viwanja vya
Mwembetogwa mjini Iringa
Asante kwa ushirikiano
……………………………………………………
Waziri wa Mambo ya
Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali ya Awamu ya
Tano imedhamiria kuwasajili watoto wote nchini wenye umri chini ya miaka
mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.
Dhamira hiyo ya
Serikali inalengo la kuiondoa nchi katika takwimu zinazoonyesha kuwa
Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho barani Afrika ambazo watoto
hawana vyeti vya kuzaliwa.
Dkt Mwakyembe amesema
hayo mjini iringa alipokuwa akizindua kampeni ya uandikishaji watoto
chini ya miaka mitano katika mikoa ya Iringa na Mbeya iliyofanyika
katika viwanja vya Mwembetogwa.
Dkt Mwakyembe ameelezea
kusikitishwa na kitendo hicho cha kuwa miongoni mwa nchi ambazo watoto
wake hawajasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa na kusema kuwa ndio
maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikaamua kuendesha kampeni
ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano.
Amesema serikali
imedhamiria kuiondoa Tanzania katika hali hiyo kwakuwa sio sahihi kwa
nchi kuwa katika nafasi hiyo sawa na Somalia
‘Hali hii sio sahihi,
Tanzania haistahili kuwepo katika kundi hilo tumedhamiria kuiondoa nchi
huko, tunataka Tanzania iwe juu ktk usajili wa watoto kama ilivyo juu
kwa chanjo mbalimbali kwa watoto wetu’ alisema.
Mpango huo ni sehemu ya
mkakati wa Serikali wa kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitano
wanasajiliwa na kuwa ma vyeti vya kuzaliwa unaendeshwa kupitia Wakala wa
Usajili, Udhamini na Ufilisi RITA chini ya ufadhili wa UNICEF.


0 comments :
Post a Comment