Msanii Juma Nature ambaye ni
mmoja wa wasanii watakaotumbuiza katika Siku ya Msanii wa Tanzania kesho
Septemba 24 kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………..
Na Herieth Semgaza
Katika kuadhimisha siku ya
msanii wa Tanzania , kwa mara ya kwanza hapa nchini Tamasha la
sikuMsanii wa Tanzania litafanyika Septemba 24 katika kijiji cha
Makumbusho jijini Dar es salaam, Siku hii itawakutanisha wasanii wa
sanaa aina mbalimbali katika jukwaa moja .
Augustino Makama ambaye ni
mratibu wa Tamasha la Siku ya Msanii wa Tanzania kutoka BASATA ametoa
ufafanuzi wa mambo kadhaa wakati akizungumza na waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam
Augustino Makama afisa sanaa
BASATA amesema kuwa siku ya msanii inawakutanisha wasanii wa sanaa ya
Mziki, Filamu, Ufundi, na Maonyesho.ilikuonyesha umahiri na uwezo wao
kwa hadhira wawapo katika jukwaa.
Aidha ameongeza Kuwa mradi huu
umebuniwa na Balaza la Sanaa la Taifa BASATA lengo lake kubwa likiwa ni
kutambua, kuhamasisha na kuthamini kazi zinazotolewana na wasanii wa
Tanzania.
Kauli mbiu ya “Nguvu ya
Sanaa”Itakayo jumuisha mtiririko wa matukio ambapo tayari maadhimisho
hayo yalishazinduliwa tangu tarehe 26 Mei 2016 na Waziri wa Habari,
Sanaa ,Utamaduni na Michezo Mh Nape Nauye.kwa uwakilishi wa katibu wa
wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel .
Maadimisho
yatafanyika katika kijiji cha Makumbusho ya Taifa Kijitonyama jijini Dar
es salaam yakidhaminiwa na kampuni ya HAAK NEEL PRODUCTION LTD
Kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 29 Ocktoba 2016 ambapo wasanii mbalimbali watapewa tuzo kutokana navigezo vilivyowekwa kwa ajili ya kupata wasanii wenye kazi bora na zenye viwango.
Kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 29 Ocktoba 2016 ambapo wasanii mbalimbali watapewa tuzo kutokana navigezo vilivyowekwa kwa ajili ya kupata wasanii wenye kazi bora na zenye viwango.
Tamasha hilo litaburudishwa na
wasanii Juma Nature, Peter Msechu, Misoji pamoja na wasaniii wengine
watakao kuwepo jukwaani ili kuwapa burudani waalikwa watakaohudhuria ,
Katika Tamasha hilo hakutakuwa na kiingilio ambapo litaanza saa tatu
asubuhi mpaka saa tatu usiku


0 comments :
Post a Comment