BINTI Karume ‘Amchana’ Lipumba

Fatma Karume, mtoto wa rais wa zamani wa Zanzibar, ameshangazwa na kitendo cha Profesa Ibrahim Lipumba  kutaka kurudi kwenye nafasi yake ya awali ya uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wakati alijiuzulu mwenyewe.

Fatma, mtoto wa Amani Abeid Karume ambaye ni rais wa sita wa Zanzibar, alisema hayo alipoulizwa kuhusu hali iliyoukumba uongozi kwenye chama hicho kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar baada ya tamko la Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa, anamtambua Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF.

Msajili huyo, Jaji Francis Mutungi alitoa uamuzi huo baada ya kuziita pande zinazosigana kwenye mgogoro, kusikiliza hoja zao baadaye kutoa maoni na msimamo wa ofisi yake kuwa Profesa Lipumba alifuta uamuzi wake kwa maandishi kabla ya mkutano mkuu wa CUF haujajadili barua yake ya kujiuzulu, hivyo anaendelea kuwa mwenyekiti halali.

“Profesa Lipumba alijiuzulu mwenyewe. Aliandika barua akaipeleka kwa katibu mkuu, kisha akautangazia umma na dunia nzima ikafahamu kwamba siyo tena mwenyekiti wa CUF,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment