Baada
ya mashabiki wa Simba kuvunja viti vya uwanja wa taifa katika mchezo wa
Simba na Yanga uliopigwa jana Jumamosi na kumalizika kwa sare ya goli
ya moja kwa moja, serikali kupitia kwa Waziri wa Michezo, Nape Nnauye
amepiga marufuku uwanja wa taifa kutumika na timu za Yanga na Simba.
Waziri
Nape amefanya maamuzi hayo baada ya leo Jumapili kufanya ziara katika
uwanja wa taifa kushuhudia uharibifu wa viti uliotokea jana, amesema
kutokana na tukio ambalo limejitokeza, kuanzia sasa michezo ya timu hizo
haitaruhusiwa kufanyika katika uwanja huo hadi pale ambapo serikali
itawaruhusu.
“Uwanja
huu hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka pale tutakapoamua vinginevyo
hapo baadae hawatatumia uwanja huu watafute viwanja vingine, sababu hapa
kuna pesa za walipa kodi, kuna pesa za watanzania,
“Wanaotakiwa
kutumia uwanja huu ukiwa mzuri kama ulivyo ni wengi kuliko Yanga na
Simba, wapo wengine ambao ni wastaarabu wanaweza kutumia uwanja huu,”
amesema Waziri Nape.
Maamuzi
mengine ni Simba kutakiwa kulipia gharama ya viti 1,781
vilivyoharibika, Simba haitapata mgao wa mchezo hadi walipe gharama za
uharibifu, kamera za CCTV zitafungwa uwanja mzima na Yanga itatakiwa
kulipa gharama ya mageti manne ya upande wa mashabiki wake yaliyovunjwa.


0 comments :
Post a Comment