Dawa
za maumivu zimetajwa kuwa chanzo cha ongezeko la vifo vya ghafla
vitokanavyo na shambulio la moyo, utafiti uliochapishwa na jarida la
kitabibu la Scientist Daily la Uingereza limebainisha.Utafiti huo
umebaini kwamba dawa za kupunguza maumivu kama Brufen zinaongeza
uwezekano wa kusababisha kifo kwa zaidi ya asilimia
20, kutokana na shambulio la moyo ‘heart attack’.Utafiti huo unashauri
kuwa ni vyema wagonjwa ambao wanaandikiwa dawa za kutuliza maumivu,
wakatumia kiwango kidogo cha dozi na kujitahidi kutozitumia mara kwa
mara.
Pia, utafiti huo umeonya wanaopenda kununua dawa hizo wakati wowote kwenye maduka bila kufuata ushauri wa daktari.



0 comments :
Post a Comment