Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea barua kutoka Shirikisho la
Mpira wa Miguu Ethiopia (EFF), ikielezea juu ya kufutwa kwa mchezo wa
kirafiki wa kimataifa uliokuwa ufanyike Oktoba 8, 2016.
EFF
imesema kwamba imelazimika kufuta mchezo huo ulikuwa kwenye kalenda ya
FIFA kwa sababu za hali ya hewa si rafiki kwa sasa nchini Ethiopia.
Kwa
barua hiyo, Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa
Stars), Charles Boniface Mkwasa atalazimika kuvunja kambi ya timu hiyo
ambayo iliweka kwenye Hoteli ya Blue Pear iliyoko Ubungo, Dar es Salaam.
Mchezo
huo uliratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za
kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. EFF, ndio
walioomba nafasi hiyo.
Ingekuwa
ni faida kwa Tanzania kama ingeshinda mchezo huo kwa maana kina alama
za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo
yake yangekuwa ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa
timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205
wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi
ya 126.
Argentina
inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa
kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki
Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani,
Colombia na Brazil.
Katika
Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo
inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.


0 comments :
Post a Comment