Wizara
ya Afya , Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto tayari imepata
chanjo ambazo zilikua pungufu hapa nchini kwa muda mrefu ambapo kwa sasa
Wananchi watapatiwa huduma hiyo kuanzia sasa huku wakiombwa Wazazi na
Walezi kupeleka watoto wao.
Kwa
mujibu taarifa zilizotolewa na Serikali kuputia Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Afya Bwana Nsachris Mwamwaja amesema kuwa chanjo
hizo zilizokuwa na upungufu mkubwa hazitasumbua upatikanaji wake kwa
sasa baada ya kuwasili nchini.
“Tutegemee
upungufu huu wa chanjo katika baadhi ya sehemu za nchi kuisha, Wizara
inawaomba Wazazi na walezi kuwapeleka watoto ambao hawakupata chanjo
wakakamilishe kupata chanjo zao.” Imeeleza taarifa hiyo kutoka kwa Mkuu
huyo wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya.
Mkuu
huyo amezitaja chanjo zilizokua na upungufu mkubwa kama zile za
upungufu za Pepopunda (T.T) na Kifua Kikuu (BCG) na akaongeza kuwa
zimewasili nchini kuanzia siku ya jana yaani Oktoba 03, 2016 na
ameongeza kuwa siku ya kesho yaani Oktoba 5, 2016 Wizara itapokea
chanjo za Polio (OPV) chanjo ambazo zinatarajiwa kusambazwa wiki hii
nchini kote.
Aidha Bw Mwamwaja amewahimiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kushiriki vyema katika utoajiwa chanjo hizo.
“Waganga
wakuu wa mikoa na wilaya kwa kushirikiana na waratibu wa chanjo
wahakikishe chanjo zinasambazwa katika vituo vyote” ameongeza Bw
Nsachris Mwamwaja katika taarifa hiyo.
Na. Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC)


0 comments :
Post a Comment