Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema
kwamba ataendelea kuwa karibu na vijana na Timu ya Tanzania ya vijana
‘Serengeti Boys’ licha ya kuondolewa na Congo kwenye harakati za kufuzu
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika
Madagascar, hapo Aprili, mwakani.
Mipango
ya TFF kwa sasa inayoongozwa na Malinzi kwa sasa ni kuiiingiza timu
hiyo kwenye program ya timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20
maarufu kwa jina la Ngorongoro Heroes baada ya kuguswa na kilio cha
vijana hao ambao walishindwa kujizuia kumwaga machozi mbele ya Malinzi
ambaye alifanya kazi kubwa kuwatuliza pamoja na viongozi wengine.
Serengeti
Boys ilipoteza mchezo dhidi ya Congo Oktoba 2, 2016. Kwa kupoteza
mchezo huo dakika ya pili kati ya nne ya nyongeza baada ya kumalizika
kwa dakika 90, kumefanya vijana hao wa Tanzania kuenguliwa kwenye
mashindano ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika –
fainali zitakazofanyika Madagascar.
Dakika
moja ndiyo iliyoipoteza Serengeti Boys kufuzu kwa fainali hizo kwa bao
la dakika ya 92 la lililofungwa na Mountou Edoward.
“Niko
nanyi, najua mna group la WhatsApp, naomba msifute namba yangu. Iwe
humo na mambo yenu mengi naomba mniambie humo, na nitayashughulikia iwe
binafsi au kiofisi. Nawahakikishia sitawaacha,” alisema Malinzi
alipowafariji vijana hao ambao wanatarajiwa kuingia leo saa 3.00 usiku
huu kwa ndege ya Shirika la Ndege ya Rwanda.
“Umri
wenu bado sana wa kucheza soka. Program za TFF, CAF na FIFA ziko nyingi
pia mnaweza kupata nafasi ya kucheza Olimpiki na kuna michuano mingi,
sitawaacha,” alisema Malinzi na kusisitiza ana imani na timu hiyo ambayo
kwa dakika 90 za mchezo dhidi ya Congo walipambana kwelikweli kutetea
taifa lao pendwa Tanzania.


0 comments :
Post a Comment