Makubaliano
hayo yamepitishwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya vyama
vinavyounga mkono serikali na baadhi ya vyama vya upinzani pamoja na
baadhi ya mashirika ya kiraia. Kwa mjibu wa ripoti ya shirika la habari
la AFP iliyotolewa na msuluhishi wa Umoja wa Afrika Edem Kodjo inaelezwa
kuwa makubaliano hayo yanatazamiwa kusainiwa leo Jumanne October 18,
2016 mjini Kinshasa na watu 300 walioshiriki katika mazungumzo.
Makubaliano hayo yaliyopitishwa katika kikao cha Jumatatu Oktoba 17, 2016 ni kuitaka Serikali kutekeleza masuala yafuatayo.
1. Tarehe ya uchaguzi
Hoja ya
kwanza ya makubaliano yaliyofikiwa na vyama vinavyounga mkono serikali
na upinzani ni kutotajwa tarehe ya uchaguzi wa urais, wabunge na
wawakilishi wa majimbo. Tarehe pekee iliyotajwa ni tarehe ya kuwasilisha
fomu za kugombea ambayo ni October 30, 2017.
Uchaguzi
mkuu utafanyika ndani ya muda wa miezi sita ambayo ni mwishoni mwa mwezi
Aprili 2018, ndivyo wajumbe wa vyama vinavyounga mkono serikali na
upinzani walivyoafikiana. Ingawa baadhi ya wajumbe wamekua wakijiuliza
kama Tume ya Uchaguzi itaheshimu tarehe hiyo mpya.
2. Waziri mkuu kutoka chama cha upinzani
Hoja ya
pili, Waziri Mkuu atateuliwa kutoka katika chama cha upinzani
kilichoshiriki katika mazungumzo. Hakuna maelezo kuhusu kugawana
nyadhifa katika serikali ya umoja wa kitaifa na Serikali itaundwa ndani
ya siku 21 baada ya kusainiwa mkataba.
3. Kamati ya ufuatiliaji
Hoja ya
tatu, kamati ya ufuatiliaji itakutana mwezi mmoja baada ya kusainiwa kwa
mkataba: wajumbe saba kutoka vyama vinavyounga mkono serikali, wengine
saba kutoka vyama wa upinzani na watatu kutoka vyama vya kiraia.
4. Ukomo wa utawala wa Rais Joseph Kabila
Hoja ya
nne, Kuhusu hatma ya rais Joseph Kabila baada ya Desemba 19, imeelezwa
kuwa Rais huyo ataendelea kubakia madarakani hadi atakapoapishwa Rais
mwengine. Makubaliano hayo yanazungumzia juu ya kuzingatia Katiba.
Hata hivyo
vyama vya upinzani ambavyo vinajumuika katika muungano wa
“Rassemblement” pamoja na baadhi ya mashirika ya kiraia ambayo yalisusia
mazungumzo hayo yametoa wito wa kumiminika mitaani Jumatano Oktoba 19.
Wakati
hayo yakijiri, Tume ya Uchaguzi ya Congo (CENI) imeruhusiwa na Mahakama
ya Katiba kuahirisha rasmi uchaguzi mkuu wakati ambao hali ya wasiwasi na hofu ya kutokea machafuko nchini DR Congo imeendelea kutanda

0 comments :
Post a Comment