Siku
kadhaa baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kutoa
maoni yake juu ya kile kinachoendelea katika Chama cha Wananchi (CUF) na
baada ya hapo wanasiasa kuwa wakitumia jina lake kwa kupinga na wengine
kukubali maoni yake, Jaji Mutungi ametoa taarifa kuhusu hilo.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya
Msajili, Monica Laurent amesema kuwa kuna watu wamekuwa wakitumia jina
la ofisi ya msajili kwa kuzungumza na vyombo vya habari na kwamba waache
tabia hiyo.


0 comments :
Post a Comment