Kamishna
wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro
leo amesema jeshi lake linawasaka mashabiki waliofanya uharibifu wa
miundombinu ikiwemo uvunjwaji wa viti katika Uwanja wa Taifa,
uliofanyika Jumamosi iliyopita katika mechi ya Simba na Yanga.
Kamanda
Sirro amesema kuwa, licha ya Waziri mwenye dhamana ya michezo, Nape
Nnauye kutoa maagizo kwa timu husika kulipa gharama za uharibifu wa
miundombinu ya uwanja huo, jeshi lake halitasita kuwatafuta waliohusika
kwa kuwa wamefanya uvunjifu wa sheria.
Amesema
Jeshi la Polisi lina mkanda wa video unaoonyesha watu waliohusika na
uharibifu huo na kwamba polisi wako katika uchunguzi ili kuwakamata
watuhumiwa hao na wakishapatikana watachukuliwa hatua za kisheria kwa
kuwapeleka mahakamani.
Aidha,
Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi limebaini kuwa wahalifu wanatumia
viwanja vya mpira kupanga mikakati ya kutekeleza uhalifu.
Amesema
hivi karibuni polisi ilifanikiwa kukamata risasi 20 za silaha ya
kijeshi aina ya G3 baada ya kubaini kundi la vijana waliokaa katika
uwanja wa Mpira wa Azam uliopo Chamanzi kuwa ni wahalifu ambapo
waliwafukuza pasipo kufanikiwa kuwakamata.
Amesema jitihada za kuwasaka wahalifu hao zinaendelea na uchunguzi wa risasi hizo unafanyika ili kubaini mahali zilikotoka

0 comments :
Post a Comment