JOSE MORINHO: MAN U INAHITAJI MUDA ILI IWE IMARA


Jose Mourinho amesema anahitaji kupewa muda zaidi ili kuitenengeza Manchester United na kuwa bora.

United wanakabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Stock City katika Uwanja wa Old Trafford Jumapili kabla ya kwenda mapumzikoni kupisha mechi za kimataifa na baadaye kurudi kukabiliana na Liverpool, Fenerbahce, Chelsea na Manchester City michezo hiyo ikichezwa ndani ya siku tisa

Na sasa akiwa tayari ameiongoza United kwenye michezo 10 tu, Mourinho amesema hatarajii kuwa amewajua kwa undani wachezaji wake pengine mpaka akae nao muda mrefu zaidi.

“Nahitahi muda. Nahitaji kuona wachezaji wangu wancheza, Nahitaji kuwaona wakiwa na utofauti mkubwa, Nihitaji kuwafahamu zaidi,” Mourinho aliwaambia wanahabari.

“Kuna mambo mengi sana ya kuangalia ili niwasome wachezaji wangu vizuri na hayo yote yatawezekna endapo nitakaa nao muda mzuri. Mara nyingi kuna utofauti kidogo unapokuwa umekaa na timu kwa miezi mitatu au minne na pengine mitano.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment