RAIS Joseph Kabila, wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), anatarajia kuwasili nchini leo kwa ziara ya siku tatu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema Rais Kabila
atapokelewa na Rais John Magufuli kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA).
Makonda aliwaambia wanahabari jana kuwa katika ziara hiyo, Kabila
atazungumza mambo mbalimbali na mwenyeji wake na kesho atatembelea
Bandari ya Dar es Salaam.
Licha ya Rais Kabila, Makonda pia alisema Makamu wa Rais wa Cuba,
Salvador Mesa ataingia nchini kwa ziara ya siku mbili na atapokelewa na
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Pia alisema katika mkoa huo kuna ugeni wa waumini wa Mabohora zaidi
ya 30,000 ambao wanafanya Mkutano Mkuu nchini baada ya kukubali ombi la
Rais Magufuli la kufanyia mkutano wao nchini.



0 comments :
Post a Comment