Serikali
imezuia fedha za mapato ya mechi kati ya Simba dhidi ya Yanga hadi hapo
gharama za uharibifu wa viti katika mechi yao dhidi ya Yanga,
itakapojulikana.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema kwamba
Simba inatakiwa kulipa gharama ya viti 1,781 vilivyoharibiwa na
mashabiki wake.
Nape amesisitiza, fedha za mapato ya Simba zitaendelea kushikiliwa hadi hapo suala la gharama ya uharibifu itakapojulikana.
Tayari kupitia Nape, serikali imetangaza kuzifungia Yanga na Simba kuutumia uwanja huo hadi hapo baadaye.
Mashabiki
wa Simba waling’oa viti wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga kwenye
uwanja huo, jana ikiwa ni baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga bao.
Tambwe
raia wa Burundi, alifunga bao hilo baada ya kuunawa mpira, jambo ambalo
lilisababisha tafrani hasa baada ya yeye kwenda kushangilia upande wa
mashabiki wa Simba.




0 comments :
Post a Comment