Nahodha
wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na kocha wa sasa wa timu ya
taifa ya vijana wadogo ya Cameroon, Rigobert Song amefikishwa
mjini Yaounde, Cameroon baada ya kuugua ghafla.
Taarifa
kutoka vyanzo vya habari vya Cameroon, zinaeleza kuwa Song amepatwa na
tatizo katika mishipa yake ya kwenye ubongo (cerebral vascular) wakati
akiwa nyumbani kwake Odza.
Baada
ya kuugua ghafla, Song alifikishwa katika Hospitali ya Messa ambapo
yupo mpaka sasa akiwa katika uangalizi maalumu wa madaktari ili
kuhakikisha anarejea katika hali yake ya awali.
MO Blog itaendelea kukuletea taarifa kuhusu hali ya mkongwe huyo wa soka barani Afrika.


0 comments :
Post a Comment