Kwa
kutambua umuhimu wa michezo kwa vijana nchini, benki ya NMB imedhamini
vijana watano kutoka nchini kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya
mashua ya Afrika yanayotaraji kufanyika Luanda, Angola kuanzia Septemba,
6-13, mwaka huu.
Akizungumzia
udhamini huo wa Milioni 10 na jezi kwa vijana hao, Mkurugenzi Mtendaji
wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema NMB kama benki ya kitanzania
inawathamini watanzania wote na inajivunia kuwa sehemu ya makampuni
ambao yameidhamini timu hiyo ili ikaiwakilishe nchi katika mashindano ya
mashua.
“NMB
ni benki ambayo inaongoza Tanzania na ipo kwa ajili ya watanzania, moja
ya sehemu ambayo tunaihudumia ni vijana, tunadhamini michezo mingi na
tunaamini ni sehemu nzuri kwa vijana wadogo maana wanatakiwa kuandaliwa
mapema,
“Mchezo
wa mashua una wachezaji wengi, NMB inajivunia kuwa sehemu ya wadhamini
kwa vijana hawa ambao watawakilishi nchi, na tunaamini watarudi kutoka
Angola wakiwa na medali,” alisema Ineke.
Nae
Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari
aliishukuru NMB kwa msaada ambao imewapatia na kuelezea changamoto
mbalimbali ambazo zimekuwa zikiukabili mchezo huo kutokana na kutokuwa
na wadhamini wanaowasimamia na kuwaomba NMB kuendeleza udhamini huo kwa
kipindi kirefu zaidi.
“Chama
chetu ndiyo kina dhamana ya kuongoza mchezo wa mashua nchini, mchezo
huu sio mgeni hata watu wanaovua ngalawa wanatumia mashua, mchezo wetu
unadumaa kwasababu hatuna udhamini na kama mnavyojua mchezo huu
unachezwa sehemu ya wazi kwahiyo hakuna anayelipa pesa, muda wote niwa
kujitolea,
“Mchezo
huu kwa sasa nchini unakuwa kama unashuka, tulianza kushiriki na watoto
12 lakini kwa sasa tunakwenda na watoto watano, mwanzo mgumu lakini
sisi tunaongeza juhudi na tunawashukuru NMB kwa hili wamelolifanya,”
alisema Nassari.
Kwa
upande wa Mwakilishi wa Dar es Salaam Yacht Club, Robert Cunnane
alisema klabu yao imekuwa ikiwasaidia watoto mbalimbali ambao wanacheza
mchezo wa mashua kwa kuwapa nafasi ya kujifunza lakini pia muda mwingine
kuwalipia fedha kwa ajili ya kwenda kujifunza mchezo huo na matarajio
ya klabu hiyo ni kuona mchezo wa mashua unakuwa maarufu nchini.
“Tumekuwa
tukisaidia mchezo wa mashua lakini kutoa udhamini kwa kutumia Milioni
24 kila mwaka kwa watoto kwenda kujifunza mchezo wa mashua na kwenda
kushiriki mashindano mbalimbali, tunajivunia kuwa na hii timu na
tunataka kuona timu hii inapata mafaikio,” alisema Cunnane.


0 comments :
Post a Comment