Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo kimeweza kuibuka na pointi tatu muhimu kibindoni baada ya kuifunga wakata Mbao wa Mkoani Mwanza, Mbao FC kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0  katika mchezo uliokuwa mkali na wa aina yake.
Simba iliwachukua mpaka dakika ya 86 kuweza kurudisha matumaini kwa mashabiki wake baada ya mchezaji wake Mzamiru Yassin kuweza kupachika bao hilo ambalo pia ndio lililokuwa la ushindi kwa Wekundu hao wa Msimbazi.
Mcheoz huo kwa Simba ni mechi yake ya 10 kwenye ligi kuu msimu wa 2016/17 dhidi ya timu hiyo ya Mbao FC, leo Oktoba 20.2016 huku ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja  tokea kuanza kwa ligi.
Kwa ushindi huo, Simba imeendelea kujichimbia kileleni kwa kujikusanyia pointi 26.