Taasisi a MO Dewji ambayo Septemba, 7 ilifanya uzinduzi wa mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi ambao watajiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (MO SCHOLAR) imetoa taarifa kwa umma sababu ya kuchelewa kutoa orodha ya majina ya wanafunzi ambao wamepata udhamini wa taasisi hiyo kwa ajili ya mwaka wa masomo 2016/2017.
TANGAZO LA MO SCHOLAR
MO Scholar inapenda kuwatangazia wanafunzi wote waliofanya usaili wa maombi ya ufadhili wa masomo ya shahada ya kwanza (MO SCHOLAR) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuwa:
1. Kutokana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu – HESLB kuchelewa kutoa taarifa na majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mkopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 hadi kufikia jana ambapo taarifa hizo zilitoka, Mo Scholar Program imelazimika kuchelewa kutoa taarifa zake za usaili na udahili wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi waliofanya maombi.
2. Mo Scholar Program inapenda kuwakumbusha wanafunzi wanaofanya maombi haya ya ufadhili wa masomo kuwa ,mwanafunzi atakayefanikiwa kupata ufadhili Bodi ya Mikopo (HESLB) hatoweza kupewa ufadhili kutoka kwa Mo Scholar Program.
3. Aidha MO Scholar Program inapenda kuwatangazia kuwa tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ya ufadhili wa masomo ni tarehe 22 Octoba 2016 (saa sita kamili usiku). 4. Majina ya washindi waliofanikiwa kupata ufadhili wa masomo wa MO Scholar Program yatatolewa na kutangazwa siku ya Jumatatu ya tarehe 24 Octoba jioni, kupitia tovuti na mitandao ya kijamii.
5. Kwa wanafunzi ambao barua pepe zao zinagoma kutuma kwenye tovuti/wavuti/barua pepe ya usaili, wanaweza kupeleka maombi yao pamoja na viambatanisho vyao katika ofisi zao zilizopo Posta, mtaa wa Ohio PSPF-Golden Jubilee Tower ghorofa ya 20.
24c7c74c-9523-47d7-909a-e681f05006ee