Taarifa
za Yanga kuingia mkataba wa kuikodisha timu kwa miaka kumi kwa Kampuni
ya Yanga Yetu zimezidi kuchukua sura mpya ambapo licha ya baadhi ya
wanachama wa klabu hiyo kupinga utaratibu uliotumika, Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) nalo limefunguka kuhusu jambo hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa
amezungumza kuhusu mabadiliko ambayo wameyafanya na kusema wao kama TFF
bado hawajayatambua mabadiliko hayo na wamemwandikia barua Katibu Mkuu
wa Yanga, Baraka Deusdedit ya kumtaka aonyesha mkataba ambao wameingia
na kampuni ya Yanga Yetu.
“Nimemuandika
barua Katibu Mkuu wa Yanga atupe nakala ya mkataba ule (wa Yanga na
Kampuni ya Yanga Yetu), ili kama kuna wasiwasi hilo tatizo
lishughulikiwe mapema maana hizi klabu niza wanachama, wanaweza kuingia
mikataba na wanachama wengine wakaja na mambo mengine,
“Tunataka
mkataba uwe wazi ili hata klabu zingine zijifunze, kwahiyo Yanga
tumewaomba walete copy ya huo mkataba nini kinaazimwa na kipi kinauzwa,
klabu itaendeshwaje na baada ya hapo kamati za TFF zitakaa kulijadili
jambo hilo, kama itakuwa tofauti na kanuni zetu tutarudi kwao
warekebishe mambo ambayo hayapo sawa,” alisema Mwesigwa na kuongeza.
“Uendeshwaji
lazima ubadilike kuendana na wakati lakini hatutaki mabadiliko
yasababishe mvurugano ambao haukuwepo kwa muda mrefu na tumeshapokea
barua nyingi za wanachama wa Yanga hadi wazee wamekuja wanasema wanataka
kwenda kumwona mkuu wa nchi”
Aidha
alisema TFF bado inatambua Yanga inasimamiwa na uongozi wa klabu kama
ilivyokuwa awali ikiongozwa na Mwenyekiti, Yusuph Manji na kama kutakuwa
na jambo la tofauti watatoa taarifa baada ya kujiridhisha mfumo ambao
Yanga itakuwa inautumia kukodisha timu kwa Kampuni ya Yanga Yetu.


0 comments :
Post a Comment