Usemi wa kuwa Ligi Kuu England sio
Ligi rahisi kuitabiri unazidi kudhihirika ikiwa ni muda mchache tu
umepita toka Man United walazimishwe sare ya 1-1 katika uwanja wao wa
nyumbani dhidi ya Stoke City, mchezo uliofuatia ulikuwa ni wa Tottenham
Hotspur dhidi ya Man City katika uwanja wa White Hatlane.
Kama ambavyo wengi walitarajia kuona Man
City akiodoka n ushindi kutokana na rekodi yake msimu huu wa kucheza
mechi sita EPL na kushinda zote, ndivyo Tottenham walivyokuwa
wamejipanga na kudhamiria kuvunja ubabe wa Man City na kuwafanya wabaki
kuwa klabu pekee msimu huu haijapoteza mchezo.
Tottenham ambao nao hawajafungwa mchezo
wowote msimu wakiwa wameishia kutoka sare mechi mbili, wamefanikiwa
kuifunga Man City goli 2-0, magoli ambayo Man City walijifunga dakika ya
9 kupitia mchezaji wao Aleksander Korarov na baadae Dele Allia akafunga
goli la pili dakika ya 37 baada ya kutumia vyema pasi ya Son Heung-Min,
Spurs walipata penati dakika ya lakini golikipa wa Man City Claudio
Bravo alifanikiwa kuokoa shuti la Lamela.


0 comments :
Post a Comment