Julio Atangaza Kuachana Na Soka Kisa Waamuzi


Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu Julio jioni ya October 2 2016 alitangaza maamuzi ya kushtushwa na wengi, hiyo ni baada ya mchezo wake wa ugenini kati ya Mwadui FC dhidi ya Mbeya City kumalizika kwa kupoteza kwa goli 1-0.
Julio baada ya mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya alitangaza kuachana na soka la Tanzania, hiyo inatokana na kutoendelea kuridhishwa na uwezo wa waamuzi wa soka wa Tanzania, kwani katika mchezo dhidi ya Mbeya City amekiri kuwa walifungwa kihalali lakini muamuzi alionesha kuwawekea vikwazo wasisawazishe.
“Mchezaji wetu anapambana hadi anapata mpira kwenda kufunga refa badala yake anatoa faulo kwao kwenye timu ya adui kusema kweli kimeniuma sana, kwa hiyo nitangaze rasmi kuanzia sasa hivi na kuendelea mimi sitaki kuwa kocha wa mpira wa miguu katika soka la Tanzania tena”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment