Baada
ya kusambaa kwa taarifa ya aliyewahi kuwa Mbunge wa zamani wa Kasulu
Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ikieleza kuwa ameamua kujiunga na
chama cha mapinduzi CCM, millardayo.com imempata Moses Machali na
amezungumza kuhusu taarifa hiyo.
“Kimsingi
ni sahihi hiyo taarifa nimeitoa mimi mwenyewe, kutokana na mwenendo wa
Serikali wa awamu ya tano, kwa mtazamo wangu na kwa ufahamu wangu kwa
rekodi za nyuma nimekuwa Mbunge ambaye nilikuwa nikipiga kelele sana
kuhusu ubadhirifu, kubana matumizi serikalini, nikiwa kama waziri kivuli
wa uchukuzi.” –
“Sasa
kwa kumuona Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa wanafanya yale
tuliyokuwa tunayataka wapinzani. Mimi nilichoamua ni kuondoka kwenye
hivi vyama vya upinzani na kwa uzoefu wangu sioni siasa zinazokua.
Nimeamua kung’atuka siku sio nyingi nitachukua kadi” – Moses Machali
Bonyeza Play hapa kupata taarifa kamili.


0 comments :
Post a Comment