Kocha wa Chelsea Antoine Conte na kiungo wake Eden Hazard wametangazwa washindi wa tuzo za EPL za mwezi October, Conte ametangazwa mshindi wa tuzo ya kocha bora wa mwezi October na Eden Hazard ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
Antoine Conte
Antoine Conte ameiongoza Chelsea
kucheza mechi nne mwezi October na kufanikiwa kushinda mechi zote nne,
wakifunga jumla ya magoli 11 na kutoruhusu kufungwa goli hata moja, huku
Hazard akifunga magoli matatu na kutoa assist ya goli moja.
Takwimu za Hazard mwezi October
Ushindi wa tuzo hiyo ya mwezi kwa Conte unamfanya kuwa kocha wa sita wa Chelsea kuwahi kushinda tuzo hiyo baada ya Claudio Ranieri, Jose Mourinho, Avram Grant, Carlo Ancelotti na Rafa Benitez.
Takwimu za jumla za Chelsea kwa mwezi October


0 comments :
Post a Comment