Mzunguko
wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara umemalizika. Timu zote 16 kwa sasa
ziko kwenye mapumziko, lakini mabenchi yao ya ufundi yakiangalia wapi
kwenye mapungufu ili kuyarekebisha.
Zipo timu zilizoonekana zina mapungufu
maeneo mbalimbali. Zipo zitakazosaka makipa, mabeki, viungo wa kati,
pembeni na hata washambuliaji. Zile klabu zenye uwezo wa kifedha kama
kawaida, zinaweza kuelekeza macho yao nje ya nchi kusaka wachezaji kwa
ajili ya usajili wa dirisha dogo.
Hata hivyo, bado zinaweza pia kuungana
na klabu zingine kusajili wachezaji toka humu humu nchini. Hadi mzunguko
wa kwanza unamalizika, kuna wachezaji walioonyesha viwango vya juu
kwenye timu zao ambao inawezekana kabisa wasiendelee kuzitumikia tena
timu zao za awali na badala yake wakasajiliwa kwingine kwa ajili ya
kuimarisha vikosi.
Hawa ni baadhi ya wachezaji ambao
kutokana na uwezo waliouonyesha, sina uhakika kama wote wanataendelea
kubaki kwenye klabu hizo, badala yake kunyakuliwa na klabu kubwa na
zenye ‘kisu kikali’.
1.Youthe Rostand-African Lyon
Ni golikipa wa timu ya African Lyon,
raia wa Cameroon. Ni mmoja kati ya makipa waliofanya vema hadi
kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi. Kwanza kabisa ana umbile la
ukipa hasa urefu, huku akiwa makini kwenye kazi yake na asiyependa
masihara. Inaonekana kama akiwa na mabeki walio makini, anaweza kuwa
mzuri zaidi ya anavyoonekana. Kutokana na uwezo wake, kuna tetesi tayari
baadhi ya klabu, ikiwemo Simba zimeanza kumnyemelea, hasa ikizingatia
kuwa mkataba wake na timu yake hiyo unaelekea ukingoni.
- Salum Kimenya-Prisons
Bado yuko kwenye kiwango kile kile cha
msimu uliopita, kilichosababisha Simba kumtolea macho, lakini
wakashindwana dau. Mechi mbili alizocheza dhidi ya Simba na Yanga,
wakidibiti mawinga hatari wa timu hizo, Shiza Kichuya na Simon Msuva,
kunamuweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutakiwa na klabu mbalimbali
kipindi hiki.
- Rashid Mandawa-Mtibwa Sugar
Ni mshambuliaji ambaye amerejea kwenye
kiwango chake cha misimu miwili iliyopita akiwa Kagera Sugar alipomaliza
ligi akiwa na magoli 10. Tayari amefunga magoli saba mpaka sasa akiwa
na timu yake mpya ya Mtibwa Sugar hadi mzunguko wa kwanza unamalizika.
Upepo ulimwendea vibaya msimu uliopita alipokuwa na Mwadui FC, akifunga
magoli mawili tu msimu mzima. Kasi yake ya ufungaji magoli inaweza
kuzishawishi timu zenye pesa kumnyakua. Mtibwa Sugar si timu yenye tabia
ya kung’ang’ania wachezaji, hivyo anaweza kupatikana kirahisi taratibu
zikifuatwa.
- Rifat Hamisi-Ndanda
Moja ya wachezaji wapya kabisa kwenye
Ligi Kuu ya Tanzania, lakini wakiwa wanakuja juu kama moto wa kifuu. Ni
kiungo mshambuliaji wa Ndanda ambaye pamoja na uchanga wake, ameondokea
kuwa mahiri na tegemeo kwenye timu hiyo. Ni mmoja wa viungo mwenye uwezo
wa kufunga magoli, kwani mpaka sasa pamoja kuiunganisha vema timu yake,
lakini ameshapachika mabao matano mpaka sasa. Huyu pia anaweza kupata
dili kwenye klabu nyingine.
- Marcel Boniventure-Majimaji
Huyu ndiye anayeifanya Majimaji kwa sasa
ipumue. Ni mshambuliaji ambaye ameshaifungia magoli matano mpaka sasa.
Japo timu hiyo ipo chini, lakini yeye binafasi ameonekana ana uwezo
mkubwa wa kufunga magoli. Na kama atapata timu kidogo yenye viungo na
matunzo bora, anaweza kuwa hatari zaidi. Ni mchezaji wa zamani wa kikosi
cha pili cha Simba. Huyu naye watu wanaweza kumnyakua mzumguko wa pili.
- Omari Mponda-Ndanda
Kuna timu ambazo zinahangaika na
mamshambuliaji. Huyu ni mmoja wa mamshambuliaji wachache wa Kibongo
wanaitingisha kwenye Ligi Kuu mpaka sasa. Ana magoli matano na uwezo
wake unaweza kuongezeka zaidi kama atakuwa kwenye timu ambayo si Ndanda.
Kumbuka ndiye aliyefunga goli la kufutia machozi, Simba ikiichapa
Ndanda mabao 31. Baada ya hapo akaanza kutupia kwenye baadhi ya mechi,
akiibeba timu yake ya Ndanda. Naona kabisa zile timu zenye uhaba wa
mamshambuliaji zinaweza kumchukua.
- Mbaraka Yusuph-Kagera Sugar
Ni mmoja wa mamshambuliaji hatari ambaye
hatupiwi sana macho na klabu mbalimbali, ikiwemo timu yake ya Simba. Ni
mchezaji aliyetoka kwenye kikosi cha pili cha timu hiyo anayechezea kwa
mkopo Kagera Sugar tangu msimu uliopita. Wakati Simba ikionekana ina
tatizo la mshambuliaji wa kati, Mbaraka ameshatupia magoli matano mpaka
sasa. Msimu uliopita akitupia magoli manane wavuni, pia akifunga
‘hattrick’ moja. Mpaka mzunguko wa kwanza msimu huu unamalizika, tayari
ameshafunga magoli matano. Mawili kati ya hayo, aliyafunga kwenye mechi
dhidi ya Yanga, Kagera Sugar ilipofungwa mabao 62. Huenda kwenye
kipindi hiki, Simba ikamrejesha kundini ili kuokoa jahazi la kukosa
mshambuliaji wa kutupia mabao, au pia kuchukuliwa na timu nyingine.
- Waziri Junior-Toto Africans
Ni mshambuliaji tegemeo wa Toto Africans
ambaye alikuwa tishio tangu msimu uliopita. Ikumbukwe ndiyo aliyeifunga
Simba kwenye mechi ya Ligi Kuu msimu uliopita na kumaliza ligi akiwa na
magoli saba. Msimu huu tayari ana magoli manne hadi kumalizika kwa
mzunguko wa kwanza Tanzania Bara. Ilikuwa bado kidogo atue Mtibwa Sugar
msimu huu, lakini ilishindikana. Baada ya mechi dhidi ya Simba, Uwanja
wa Uhuru, kiongozi mmoja mwadui FC aliongea naye akiahidi kuwa anaweza
kumchukua kwenye timu yake kipindi cha dirisha dogo.
- Kelvin Sabato ‘Kiduku’-Stand United
Ni mshambuliaji wa kwanza kufunga
‘hattrick’ msimu huu. Alifanya hivyo, timu yake ya Stand United
ilipoichapa Mtibwa Sugar mabao 32. Amefunga magoli manne mpaka sasa
kwenye Ligi Kuu. Ni mshambuliaji msumbufu ambaye ameifanya Stand kuwa ya
kutisha msimu huu, akisajiliwa kutoka timu hasimu ya Mwadui
aliyeipandisha Ligi Kuu. Pia anaweza kutoihudumu timu hiyo, kama watu
watafika bei kutokana na kiwango chake.
- Ally Nassor ‘Ufudu’-Kagera Sugar


0 comments :
Post a Comment