Afisa Habari wa Azam FC Jafar Idd
amethibisha ushiriki wa klabu hiyo katika michuano ya Mapinduzi Cup
inayotarajia kuanza December 30 hadi January 13 visiwani Zanzibar.
Jafar Idd ametaja malengo ya
mwalimu wa timu yao kushiriki michuano hiyo ambayo lengo lake ni
kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar kila Jarury 12.
Maandalizi ya michuano ya kimataifa
“Ni michuano ambayo kwetu sisi
Azam FC tunaiona dhahiri shahiri kwamba ni sehemu yetu ya maandalizi ya
michuano ya kimataifa na mwendelezo wa ligi kuu Tanzania bara ambao
tunaendelea nao sasa hivi.”
Kujaribu wachezaji wapya
“Kuna baadhi ya wachezaji ambao
tumewasajili msimu huu kutoka nje ya nchi na wengine wakiwa ni wa hapa
nyumbani, kwahiyo itakuwa ni changamoto yao kuonesha uwezo wao katika
michuano hii ya Mapinduzi Cup.”
“Tupo kundi moja na Yanga na hii
ni mara ya pili mfululizo inatokea tunakutana nao kwenye kundi moja,
tunaamini kuwa kundi letu litakuwa ndio lenye ushindani mkubwa, kila mtu
anafahamu kuwa tunapokutana na Yanga aina ya mpira inakuaje na presha
inakuaje kwa mashabiki, kwa hiyo ni matarajio yetu kutakuwa na ushindani
mkubwa”.
Katika malengo yote yaliyotajwa na
Jafar Idd, hakuna lengo la kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ambapo Azam
ni washindi mara mbili wa kombe hilo ((2012, 2013).
Azam FC ipo Kundi B, kundi moja
na Yanga, Zimamoto na Jamahuri, Azam itacheza mechi yake ya kwanza
Januari 2 kwa dhidi ya Zimamoto kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.
0 comments :
Post a Comment