Kocha
Mkuu wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa itakuwa
vigumu kwa kikosi chake kushindana na viongozi wa ligi ya Uingereza
Chelsea.
City ilipanda hadi nafasi ya pili
katika jedwali baada ya kuicharaza Hull City 3-0 katika siku kuu ya
Boxing Dei na kuweza kuwa nyuma ya Chelsea kwa pointi 7.
Kikosi hicho cha Antonio Conte
awali kiliweka rekodi ya kushinda mara 12 katika ligi ya Uingereza baada
ya kuichapa Bournemouth 3-0.
”Tumecheza mechi saba zaidi ya Chelsea ,ndio maana ni vigumu ”,alisema Guradiola.
”Liverpool ilikaribia taji hilo
mwaka mmoja uliopita kwa sababu walikuwa na mechi moja kwa wiki ,na ni
hivyo ndivyo ilivyokuwa na Leicester.Mara hii Chelsea na Liverpool wana
fursa”.
Liverpool na Chelsea zilishindwa
kufuzu katika mashindano ya Ulaya baada ya kumaliza wa nane na 10
mtawalia katika ligi ya Uingereza mwaka uliopita.
0 comments :
Post a Comment