Wanahabari wakiwa wamebeba jeneza
lenye mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian,
marehemu Mpoki Bukuku baada ya kutolewa heshima za mwisho katika Uwanja
wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam, tayari kulisafirishwa
kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwaongoza waombolezaji kutoa heshima za
mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian,
marehemu Mpoki Bukuku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es
Salaam. Mwili wa Mpoki ulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa
mazishi.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya
Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa akiwa ameshika shada la maua alipokuwa
akiingiza kwenye gari lenye jeneza la mwili wa marehemu Mpoki Bukuku
Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la
Jambo Leo ambaye pia ni Mmiliki wa Blog hii, Richard Mwaikenda akitoa
salamu za rambirambi za Chama cha Mabloga Tanzania (TBN) wakati wa kuaga
mwili wa mpendwa Mpoki Bukuku.
Mwakilishi wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Habari Tanzania (MOAT), Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi
Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akitoa salamu za rambirambi
Mwakilishi wa Chama cha
Wapigapicha za Habar Tanzania (PPAT), Selemani Mpochi akitoa salamu za
rambirambi. Mpoki alikuwa mwanachama wa chama hicho.
ADMIN wa Group la WhatsApp la
Tasnia, Thomson Kasenyenda akita salamu za rambirambi na kuahidi group
hilo kuwasilisha mchango wao kwa kulipia ada za shule za watoto wa
marehemu
Mwenyekiti wa Chama cha Bongo Movie, Steven Nyerere akitoa salamu
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi
wa Habari za Michezo na Burudani Tanzania (TASWA), Juma Pinto akitoa
heshima za mwisho kwa mwili wa Mpoki Bukuku.
Benny Kisaka akitoa heshima za mwisho
Mhariri Mtendaji wa The Guardian, Mgamba akitoa heshima za mwisho
Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Muhidini Issa Michuzi akitoa heshima za mwisho
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mpoki Bukuku
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete akitoka kutoa heshima za mwisho
Mpigapicha wa The Guardian na Nipashe akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho
Mpigapicha wa zamani wa Daily News, Athuman Khamisi akitoa heshima za mwisho
Mtoto wa kike wa maraehemu Mpoki Bukuku akimvalisha Rozali wakati wa kuaga mwili wa babake
Mjane wa marehemu Lillian akiubusu mwili wa mumewe
Mtoto wa kiume wa marehemu Mpoki Bukuku, Junior akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa babake
Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Msalato Dodoma kwa mazishi.
0 comments :
Post a Comment