Beki wa Chapecoense ya Brazil Alan Raschel aliyenusurika katika ajali ya ndege November 29 2016 Colombia walipokuwa wanaelekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Club Bingwa America Kusini dhidi ya Atletico Nacional, ameonekana uwanjani kwa mara ya kwanza.
Raschel ni miongoni mwa watu sita walionusurika katika ajali iliyoua watu 71 wakiwemo na waandishi wa habari, December 22 2016 Raschel alihojiwa na kituo cha TV cha Brazil na kueleza kuwa mchezaji mwenzake Jackson Follman alisaidia kunusuru maisha yake.
“Kabla
ya kuanza safari Jackson Follman aliniomba nibadili siti na kukaa nae
pamoja na mimi nilimsikiliza, kwa heshima yake kwa sababu nimefahamiana
na Follman toka 2007, nikahama pale na kwenda kukaa nae kumbe kufanya
vile kulisaidia kuokoa maisha yangu kutoka nilipokuwa nimekaa”
Jackson Follman ambaye ni golikipa wa Chapecoense
ni miongoni mwa watu 6 waliyonusurika katika ajali, lakini imeripotiwa
kuwa hatoweza kurudi uwanjani na kucheza soka kutokana na kuumia mguu na
kupelekea kukatwa, lakini Chapecoense imemuahidi kumpa kazi katika kipindi chote cha maisha yake.
0 comments :
Post a Comment