Wabunge wa chama tawala nchini Kenya, wameifanyia marekebisho sheria ya Uchaguzi ikiwa ni miezi nane imebakia kuelekea Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais unatarajiwa kufanyika mwaka 2017.
Kwa mujibu
wa Bunge la Kenya, mabadiliko hayo yataiwezesha Tume ya Uchaguzi nchini
humo kutumia njia ya kawaida kuwatambua wapiga kura na kuwasilisha
matokeo ya Urais ikiwa mfumo wa teknolojia hautaweza kufanya kazi yake
vizuri.
Wabunge wa
upinzani nchini humo wamepinga mabadiliko hayo na baada ya kuona
hawasiliziwa waliamua kutoka bungeni wakati wa mjadala wa kuirekebisha
sheria hiyo ukiendelea, wabunge hao wamedai kuwa wabunge wa serikali
walikuwa wamejiandaa kwa silaha hatari ili wawadhuru..
Aidha,
upinzani unadai kuwa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta imebadilisha sheria
hiyo ili kutengeneza mazingira ya kuiba kura, madai ambayo serikali
kupitia wabunge wa chama tawala wamekanusha na kueleza kuwa mabadiliko
hayo yataipa nafasi Tume ya Uchaguzi kutumia mfumo mbadala ikiwa
mtandao utasumbua siku ya kupiga kura mwezi Agosti mwaka ujao.
Baada ya
marekebisho hayo kupitishwa, Mahakama imesema haiwezi kuzuia kikao cha
bunge kuendelea kwa sababu mabadiliko hayo bado hayajawa sheria. Taarifa
ya upinzani inasema watahakikisha
kuwa Uchaguzi wa mwaka 2017 haufanyiki kutokana na kufanyika kwa
mabadiliko hayo na hata kutishia kuwepo kwa maandamano nchi nzima.
0 comments :
Post a Comment