Serikali imesema kumeibuka upya kwa ugonjwa wa kipindu pindu katika mikoa sita ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wapo wagonjwa 458 huku sita wakiwa wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu aliitaja mikoa yenye wagonjwa wa kipindipindu kuwa ni pamoja na Morogoro wagonjwa 282 na Dodoma wagonjwa 96.
Aliitaja mikoa mingine kuwa ni Mara wagonjwa 31, Kigoma wagonjwa 30, Arusha 11 na katika jiji la Dar es salaam wapo wagonjwa 8 wa kipindupindu kati ya hao 6 kutoka Ubungo na 2 kutoka Ilala.
Aidha, Mh. Waziri amebaini kuwepo kwa uzembe mkubwa unaofanyika katika wilaya na mikoa kwa kushindwa kutoa taarifa za ugonjwa huo huku wagonjwa wa kipindu pindu wakilazwa pamoja na wagonjwa wa kawaida kwa kile kinachoelezwa ni viongozi kuogopa kutumbuliwa na Rais Dkt. John Magufuli
0 comments :
Post a Comment