Geofrey Nyange mesema wachezaji wakuachwa kwenye kikosi chao cha msimu ujao wanatarajia kuwatangaza hivikaribuni lakini hakuna jina la Mavugo
Makamu wa rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema hata kama wakimpata Donald Ngoma hawatomwacha mshambuliaji wao Laudit Mavugo.
Kaburu ameiambia Goal lengo lao ni kuimarisha kikosi chao na kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo unaofanana hivyo kumuacha Mavugo ni sawa na kukidhohofisha kikosi chao na kufanya kiwe tegemezi.
“Tunachotaka mchezaji wa ndani na aliyeanzia benchi wote wawe na viwango sawa na ndiyo maana tunamsaka Ngoma lakini tutaendelea kuwa na Mavugo kwa sababu ni mchezaji muhimu kwetu,” amesema Kaburu.
Kiongozi huyo amesema wanataka kuwa na kikosi kipana ambacho kitakuwa na ushindani baina ya mchezaji na mchezaji jambo ambalo litasaidia hata kupatikana kwa mafanikio.
Amesema wachezaji wakuachwa kwenye kikosi chao cha msimu ujao wanatarajia kuwatangaza hivikaribuni lakini hakuna jina la Mavugo.
“Mavugo amekuwa na mchango mkubwa kwetu hilo halina ubishi ameweza kufunga mabao saba ni rekodi nzuri ingawa bado anatakiwa kuongeza juhudi ili kumfikia Shiza Kichuya na wengineo,” amesema.
Simba tayari imemsajili John Bocco na sasa inapambana na Ngoma ili kuiongezea kasi safu yao ya ushambuliaji ambayo imepungukiwa na mshambuliaji mmoja Ibrahim Ajibu aliyejiunga na Yanga
0 comments :
Post a Comment