VPL:KIUNGO WA YANGA JUSTINE ZULU ‘MKATA UMEME’ASHINDWE MWENYEWE TU


zulu_01
Kiungo Justice Zulu maarufu kama “Mkata Umeme”, anaweza kuanza kucheza katika mechi zinazofuatia za Yanga.
Suala la kutumika kwa Zulu litakuwa ni la Kocha George Lwandamina kwa kuwa sasa kila kitu safi.
Tayari uongozi wa Yanga umelishughulikia suala la vibali vya mchezaji huyo, hasa kile cha kufanya kazi nchini ambacho awali hakikuwa kimekamilika.
Lakini mwenyewe anaonekana kuwa yuko fiti tayari kwa mechi kwa kuwa amekuwa akiendelea kufanya mazoezi binafsi kuhakikisha anakuwa fiti zaidi.
Zulu amejiunga na Yanga akitokea Zesco ya Zambia, lakini kabla hakuwa amecheza mechi ya mashindano kwa zaidi ya miezi minne.
Kutokana na hali hiyo, ameonekana kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuhakikisha anafanikiwa kurejea katika kiwango chake.
Kabla, Yanga ilimpanga katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa kwanza lakini suala la kukosa kibali cha kazi, ilichangia aondolewe kwenye listi katika dakika za mwisho kabisa.
Yanga wanatarjia kushuka kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kucheza na timu ngumu kwao Ndanda FC ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment