Kocha mkuu wa timu ya Ashanti
United ya jijini Dar es salam,Maalim Salehe amesema kwamba shirikisho la
mpira wa miguu hapa nchini limeendelea kushindwa kuendesha kwa weledi
mpira wa miguu hapa nchini akidai kuwa kwa mara nyingine wameshindwa
kutenda haki katika utoaji wa ratiba ya michezo ya kombe la FA.
Salehe amesema kwamba kama kocha
mkuu wa timu ya Ashanti anashangaa kuona ratiba yao inaonyesha kuwa siku
ya kesho wanacheza na Yanga mechi ya FA pasipo mpangilio mzuri wa
utoaji wa taarifa kwa wahusika.
Amesema kwamba kwa upande wake
tayari kwa siku ya jana alishawapa mapumziko mafupi wachezaji wake kwani
alikuwa hafahamu kama siku ya kesho watakuwa na mechi tena
ikiwakutanisha na timu kongwe hapa nchini.
“Ndugu mwandishi mimi taarifa za
mechi nimepata leo asubuhi,hapo hapo jana niliwapa mapumziko wachezaji
wangu maana nimeona ni vyema baada ya mazoezi magumu niwape mapumziko
mafupi sasa kwa sasa sina jinsi itabidi tupeane taarifa turejee wote
kambini”alisema Maalim Salehe.
Hata hivyo amedai kuwa ingawa
ratiba hiyo si rafiki kwao lakini hapo kesho wanataraji kushika dimbani
kucheza mchezo huo unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar
es salaam kuanzia mishale ya saa kumi kamili jioni.
0 comments :
Post a Comment