Na: Frank Shija – MAELEZO
ELIMU bure yaongeza idadi ya
udahili wa wanafunzi wa shule za msingi nchini waongezeka kutoka
1,282,000 mwaka 2015 hadi kufikia 1,896,000 mwaka 2016 ambayo ni sawa na
ongezeko la asilimia 84.5.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu
wa Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe alipokuwa anaongea katika kipindi cha tunatekeleza
kinachoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO na kurushwa na Televisheni
ya Taifa (TBC1) jana jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa
dhamira ya Serikali nikuhakikisha inatoa huduma bora za kijamii ikiwemo
elimu, afya, miundombinu na maji safi.
“Dhamira ya Serikali ni kutoa
huduma bora za afya,elimu,maji na miundombinu ndiyo maana Serikali ya
Awamu ya Tano ikaja na Sera ya Elimu bure ili kutoa fursa kwa wananchi
wake kupata elimu,”alisema Mhandisi Iyombe.
Aidha Muhandisi Iyombe amebainisha
kuwa kazi kubwa ya TAMISEMI ni kuratibu na kusimamia Mikoa, Wilaya na
Halmashauri katika utoaji wa huduma bora za maendeleo kwa wananchi.
Aliongeza kuwa ili Serikali iweze
kutimiza azma yake ya kuwapatia huduma za maendeleo wananchi wake
imeweka mfumo dhatibiti wa ukusanyaji wa mapato katika halmashauri
nchini ili kuhakikisha fedha inapatika kiwa ajili ya kutekeleza miradi
ya maendeleo.
Mhandisi Iyombe amesema kuwa
mapato yanayokusanywa na halmashauri nchini ni kwa ajili ya kutoa huduma
za kimaendeleo ili wananchi wanufaike.
0 comments :
Post a Comment