Kocha Avram Grant amewaacha
wachezaji wake katika hali ya huzuni mkubwa baada ya kuwaambia kuwa
wakati wake wa kuinua Ghana utamalizika baada ya Michuano ya Mataifa
Afrika ‘AFCON’ inayoendelea nchini Gabon.
Kocha huyu mwenye umri wa miaka 61
ambaye mkataba wake unamalizika baada ya Michuano hii amesema “Nilikuja
kwa ajili ya miaka miwili Ghana,tuliongeza miaka miwili na miezi mitatu
kwa sababu tulifuzu AFCON”
Hata hivyo mpaka sasa Ghana tayari
wamefuzu robo Fainali na kama kocha huyu akiiongoza Ghana kutwaa
ubingwa na kuhitimisha miaka 35 ya ukame wa AFCON,basi atakuwa amewaaga
vyema Waghana.
0 comments :
Post a Comment